Ads

Mahakama yatupilia mbali pingamizi la Madonna kuhusu Barua ya Tupac

Msanii wa maarufu wa muziki wa pop Madonna ameshindwa kwenye kesi ya kumzuia rafiki yake wa zamani Darlene Lutz kutouza barua za kuvunjika kwa uhusiano wa kimapenzi kati yake na marehemu Tupac Shakur, ikiwemo kuachana.
Jaji wa New York ambaye alikuwa akisikiliza kesi hiyo alitupilia mbali kesi ya Madonna dhidi ya Darlene Lutz akisema kuwa muda umeshapita wa kuipata hiyo barua ya kuvunjika kwa uhusiano kati yake na msanii Tupac Shakur aliyefariki 1996 ambaye alikuwa na uhusiano wa kisiri na Madonna.
Kwa mujibu wa mtandao wa TMZ mnada huo sasa utafanyika mwezi July na ikumbukwe kwamba Madonna aliwahi kudai kwamba hakujua kwamba Lutz alikuwa akimiliki barua za Tupac alizoandika 1995 hadi aliposikia kuhusu mnada huo wa mtandaoni mwaka uliopita.

No comments

Theme images by andynwt. Powered by Blogger.